Mkutano wa pili wa shughuli za utalii wa nchi zinazoendelea
umefanyika jana mjini Zanzibar, Tanzania, na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi
15 zikiwemo Marekani, Uingereza, Kenya, na Korea Kusini.
Kwenye mkutano huo, waziri wa habari, utalii na utamaduni wa
Zanzibar Said Ali Mbarouk amesema, ni muhimu kwa nchi zinazoendelea kuandaa
mkakati wa maendeleo ya sekta ya utalii katika miaka 20 ijayo.
Amesema nchi zinazoendelea zinapaswa kuwa na mazingira mazuri,
ufundi na utamaduni vitakavyowavutia watalii na kuwataka washiriki wa mkutano
huo waweze kuthibitisha mwelekeo wa maendeleo endelevu katika sekta ya utalii.
Mkutano wa kimataifa wa utalii katika nchi zinazoendelea
unafanyika kila baada ya miaka miwili, na unajadili matokeo ya utafiti na
uzoefu kwenye shughuli za utalii, ili kutafuta njia ya kutatua changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo katika nchi zinazoendelea..
No comments:
Post a Comment