Thursday, August 9, 2012

MAHALU ASHINDA KESI YAKE


Aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia Profesa Costa Mahalu hii leo katika MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, ameshinda kesi Uhujumu Uchumi na Kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2 milioni, iliyokuwa ikimkabili.
Balozi Mahalu na aliyekuwa  Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin  walikuwa wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, katika mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Wadadisi wa mambo hapa nchini wanasema huenda ushindi huo wa Balozi mahalu, aliyekuwa akitetewa na wakili Mabere Marando, umechangiwa na ushahidi uliomtetea kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

No comments: