Tuesday, August 14, 2012

KAMA ULIDHANI NI KIGAMBONI PEKEE..... BASI SIO SIKIA VURUGU HILI LA POLISI NA WANANCHI MTWARA LEO....

Mabomu ya machozi yatumika

Wananchi walalamika polisi wanawaonea
Mali zao zaharibiwa , tv simu , maduka vurugu
Mkuu wa polisi wilaya asema bado anafuatilia kujua nini kimetokea
Mkuu wa wilaya akiri kutokea, asema amewaagiza watu wa usalama wampatie taarifa kamili

Mkoani Mtwara.... leo hii kumetokea vurugu baina ya askari polisi na wananchi wa mtaa wa ZIWANI.

Vurugu hizo zilizuka baada ya polisi waliodaiwa kuweka mtego kuwanansa vijana wanaohusika na wizi wa mafuta kutoka katika makampuni yaliyopo hapa mkoani mtwara.

Inadaiwa kuwa baada ya

 polisi kufika eneo hilo walimtaka kiongozi wa serikali ya mtaa.... kuwaongoza hadi kwenye nyumba iliyokuwa inadaiwa kuwa na mafuta hayo.

Baada ya kiongozi huyo kukataa kufanya hivyo kwa madai kuwa wapo wenye mamlaka zaidi ya yeye, inadaiwa polisi waliamua kwenda kwenye nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo na kisha kuanzisha msako...

wakati vurugu hizo zikiendelea wananchi waliamua kuingilia kati, na kisha inasemekana wakampiga jiwe kichwani askari mmoja na kuiharibu simu yake ya upepo (radio call) kilichotokea, baadae, polisi wakaita wenzao na kisha kichapo kikaanzakuetmebea..

Mkuu wa wilaya amethibisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa bado anafuatilia taarifa zaidi, na kisha ataziweka hadharani nini hasa kimetokea.......

No comments: