Wednesday, August 1, 2012

JANA ASUBUHI.... AJALI YA MABASI MAWILI , BARABARA YA KUELEKEA MKOANI MTWARA...MKURANGA ENEO LA SHELI YA MURO

Ajali hiyo ilihusisha basi la WIFI lenye namba za usajili T 930 BFZ lilokuwa likielekea Ruangwa na basi la CAMPAS lenye namba za usajili T 637 AZX, lilokuwa linaelekea mkoani Mtwara....Hakuna mtu aliepoteza maisha hadi mwandishi anaondoka katika eneo la tukio... mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari la Campas aliumia sehemu za miguuni. Mwanausalama akizungumza na abiria waliokumbwa na dhahama.
 Sehemu ya abiria waliopatwa mshtuko baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kugongana.
 Wasamaria wema wakijaribu kumuokoa abiria wa basi la Campas, aliekuwa amebanwa vibaya sehemu za miguu. Abiria huyu alikuwa seat ya kwanza.

Huyu ndio abiria aliekuwa amebanwa vibaya sehemu za miguuni.

No comments: