Saturday, July 7, 2012

WAZANZIBAR WALIOKIMBILIA SOMALIA WAREJEA

Picture
Wazanzibari waliokuwa wakiishi Somali kama wakimbizi wamerejea nyumbani jana na kupokelewa na ndugu na jamaa zako katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Hali ya ulinzi ulikuwa imeimarishwa na maafisa wa usalama ambapo haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari na wapiga picha kuwasogela hadi walipotoka ndani ya ndege mbili maalumu za Umoja wa Mataifa (UN) zilizowaleta.


Sura za wa wageni hao na wapokeaji zilisajika baada ya kufika uwanja huo ambapo baadhi ya watoto wakionekana wakilia muda mfupi baada ya kutua huku wazazi wao wakiwa na furaha na kukanyanga tena nyumbani.Wakizungumza na waandishi wa habari walionesha hisia zao za kufuwahia kurudi nyumbani na kusikitika kuwa baadhi ya wenzao wamekataa kurudi kutoka na kupata taarifa za maandamano yaliotokea Mei 27 mwaka huu na kusababisha mali kuharibiwa na baadhi ya watu kushitakiwa.“kwa kweli watu wengi walikuwa tayari kujisajili na UNHCR tayari kurudi nyumbani lakini kitu kilichowarejesha nyuma wenzetu ni baada ya kusikia maandamano na baadhi ya matukio ya hivi karibuni kuzuwiwa kwa mihadhara na baadhi ya watu kushitakiwa….kwa hivyo wakaogopa akiamini hali haijatulia bado” alisema Mohammed Suleman na kuongeza.

SOMA ZAIDI...ZANZIBAR YETU

No comments: