Tuesday, July 10, 2012

THOMAS LUBANGA AHUKUMIWA

Thomas Lubanga katika mahakama ya ICC


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imemhukumu Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Union of Congolese Patriots la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Hakimu Adrian Fulford aliitangaza hukumu ya Lubanga na kueleza kwamba mshtakiwa huyo atakwenda jela kwa miaka 8 tu kwa sababu ameshakaa rumande tangu mwaka 2006. Lubanga mwenye umri wa miaka 51 amehukumiwa kwa kosa la kuwateka watoto wadogo, baadhi yao wakiwa na umri wa miaka 11 tu, na kuwatumia kama maaskari katika kundi lake la waasi. Hata hivyo hakimu Fulford amesema kwamba mahakama imeshindwa kuthibitisha kwamba Lubanga alihusika katika shutuma za unyanyasaji wa kijinsia.
Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC, akishtakiwa kwa makosa kadha wa kadha yanayokiuka kahi za binadamu. Tarehe 14 mwezi Machi mwaka huu, mahakama ilitangaza kwamba Lubanga amekutwa na hatia ya kuwakamata watoto na kuwatumia kama maaskari katika mapambano yaliyofanyika kwenye eneo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kati ya mwaka 2002 na 2003.SOMA ZAIDI... BOFYA HAPA

No comments: