Thursday, July 12, 2012

TATIZO LETU NI LIPI HATUJIFUNZI..... 100 WAFARIKI HUKOO NIGERIA

Lori la mafuta
Zaidi ya watu mia moja wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kuanguka kusini mashariki mwa nigeria katika Jimbo la Delta.
Wakuu wa Serikali wanasema kuwa wenyeji wa eneo hilo walikimbilia kuzoa mafuta yaliokuwa yakichuruzika toka lori hilo lakini likalipuka na na kusababisha maafa hayo.
Mwandishi wa habari Emeka Idika ameiambia BBC kuwa mazishi ya halaiki kwa watu waliofariki kutokana na moto na wasioweza kutambulika yatafanywa katika Jimbo la Rivers wakati wengine wapatao 35 wamelazwa katika hospitali

No comments: