Thursday, July 12, 2012

NDUNGULILE ATOLEWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE NI KWA KUGOMA KUTHIBISHA SHUTUMA ZAKE DHIDI YA MADIWANI WA KIGAMBON

Mbunge wa jimbo la kigamboni, Dkt Faustine Ndungulile jioni hii ametimuliwa nje ya ukumbi wa bunge baada ya yeye kukataa kuomba radhi ama kuthibitisha tuhuma zake juu ya madiwani wa Kigamboni kuwa walihongwa.
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai jioni hii amemtoa nje Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dk Faustine Ndugulile baada ya kukaidi kutoa ushahidi wa tuhuma za Waziri Tibaijuka kuwaonga madiwani wanne wa Kigamboni.

Tuhuma hizo zinadaiwa alizitoa jana wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Ndugai alimtaka Mbunge huyo kufanya moja wapo kati ya mambo mawili, atoe ushahidi wa madai yake hayo ama akishindwa basi aombe radhi kitu ambacho Mbunge huyo hakukifanya.
"Kwa mujibu wa Kanuni 73:3 ambayo inasema kuwa iwapo mbunge hajathibitisha tuhuma azozitoa bungeni hata baada ya kupewa nafasi ya kufanya hivyo ni kutolewa nje na kutohdhuria vikao vitatu vya bunge", alisema Ndugai huku akiwataka askari kumsindikiza Dk Ndugulile hadi mwisho wa lango la Bunge.

No comments: