Thursday, July 5, 2012

HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO WAMAENDELEO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2012/2013


A.    UTANGULIZI
1.          Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango wa Maendeleo na Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 

2.          Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kushiriki katika Mkutano huu wa Bunge unaojadili Bajeti ya Serikali.


B:    MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2011/12

3.          Mheshimiwa SpikaWizara ya Ujenzi ina jukumu la kusimamia sekta ya ujenzi ambayo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji na maendeleo ya sekta za kiuchumi na kijamii nchini. Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2011/12 ulizingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010; ahadi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Sera na Sheria; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025; MKUKUTA;  Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Miundombinu ya Uchukuzi (Transport Sector Investment Program – TSIP); na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millennium Development Goals- MDGs).

UKUSANYAJI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAWAIDA


4.          Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/12, Wizara ilitengewa shilingi 245,440,294,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 7,974,670,219.00 zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, na mishahara shilingi 15,829,643,781.00.  Hadi kufikia Juni, 2012, Shilingi 242,004,520,900.00 sawa na asilimia 98.60 ya bajeti zilitolewa na HAZINA kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 16,763,849,878.00 ni mishahara ya watumishi wa Wizara na Taasisi, shilingi 221,585,980,000.00 ni fedha za Mfuko wa Barabara sawa na asilimia 100.00 ya bajeti na shilingi 3,654,691,071.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo ya Wizara na Taasisi. Aidha, kupitia Idara ya Utawala; Idara ya  Huduma za Kiufundi na Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi; hadi Juni, 2012, jumla ya shilingi 16,606,114.09 zilikuwa zimekusanywa.

 

MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/12


5.    Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2011/12 Wizara  ilitengewa shilingi 1,155,976,936,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo shilingi 526,106,746,000.00 zilikuwa ni fedha za ndani na shilingi 629,870,193,000.00 zilikuwa ni fedha za nje. Fedha zilizotolewa hadi Juni, 2012 ni shilingi 865,037,320,000.00.  Mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Mwaka 2011/2012 mradi kwa mradi imefafanuliwa kwa kirefu katika kitabu cha hotuba yangu.

GHARAMA ZA MIRADI INAYOENDELEA

6.          Mheshimiwa Spika, kwa ujumla miradi mikubwa ya barabara, madaraja, vivuko, nyumba na majengo ya Serikali inayoendelea kutekelezwa na Wizara ya Ujenzi ambayo imeenea nchi nzima ina thamani ya shilingi bilioni 6,005.63653 (Trilioni 6 na bilioni 5.63653) kama inavyoelezwa hapa chini (miradi mingine midogo inayoendelea katika nchi nzima haihusiki na takwimu hizi).

7.          Mheshimiwa Spika, miradi mikubwa ya barabara inayoendelea kutekelezwa katika mkoa wa Mtwara na Ruvuma ina jumla ya shilingi bilioni 592.0583. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara za:-


(i)          Masasi – Mangaka (km 54): shilingi bilioni 21.62
(ii)        Mangaka – Tunduru/Mtambaswala (km 202.5): shilingi bilioni 240.858
(iii)      Tunduru – Matemanga (km 58.70): shilingi bilioni 63.41
(iv)      Matemanga – Kilimasera (km 68.20): shilingi bilioni 64.02
(v)        Kilimasera – Namtumbo (km 60.70): shilingi bilioni 53.23
(vi)      Namtumbo – Songea (km 67.00): shilingi bilioni 62.88
(vii)    Peramiho – Mbinga (km 78.00): shilingi bilioni 79.81
(viii)  Mbinga – Mbamba Bay (km 66.00): shilingi bilioni 2.90
(ix)      Makambako – Songea (km 295): shilingi bilioni 0.979
(x)        Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200): shilingi bilioni 0.779
(xi)      Daraja la Nangoo; shilingi bilioni 0.578
(xii)    Daraja la Umoja: shilingi bilioni 0.2943
(xiii)  Mtwara – Newala – Masasi (FS & DD) (km 209): shilingi bilioni 0.70

8.          Mheshimiwa Spika, katika mkoa wa Tabora na Kigoma, barabara ya Kigoma – Kidahwe na barabara ya Mwandinga – Manyovu zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Miradi ya barabara na madaraja inayojengwa na Serikali kwa sasa ina thamani ya shilingi bilioni 623.02565. Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Kidahwe – Kasulu – Nyakanazi (km 300): shilingi bilioni 3.50:
(ii)        Kidahwe – Uvinza (km 76.60): shilingi bilioni 78.24
(iii)      Daraja la Mto Malagarasi (Daraja la Kikwete) na barabara zake (km 48): shilingi bilioni 78.91
(iv)      Tabora – Ndono (km 42): shilingi bilioni 51.35
(v)        Ndono – Urambo (km 52): shilingi bilioni 59.77
(vi)      Urambo – Kaliua – Ilunde (km 146): shilingi bilioni 2.50
(vii)    Tabora – Sikonge (km 70): shilingi bilioni 1.00
(viii)  Tabora – Nyahua (km 85.00): shilingi bilioni 93.41
(ix)      Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.40): shilingi bilioni 109.64;
(x)        Mwandiga – Manyovu (km 60): shilingi bilioni 0.86565
(xi)      Nzega – Puge (km 56.10): shilingi bilioni 66.36;
(xii)    Puge – Tabora (km 58.80): shilingi bilioni 62.74
(xiii)  Ipole – Koga – Mpanda (km 273 ): shilingi bilioni 1.20
(xiv)  Daraja la Mbutu: shilingi bilioni 12.34

9.          Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Rukwa na Katavi, miradi ya jumla ya shilingi bilioni 587.69 inatekelezwa na Wizara ya Ujenzi katika ujenzi wa kiwango cha lami. Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Tunduma – Ikana: (km 63.70): shilingi bilioni 82.52;
(ii)        Ikana – Laela (km 64.20): shilingi bilioni 76.10;
(iii)      Laela – Sumbawanga (km 95.10): shilingi bilioni 130.10;
(iv)      Sumbawanga – Kanazi (km 75.00): shilingi bilioni 78.84;
(v)        Kanazi – Kizi – Kibaoni (km 76.60): shilingi bilioni 82.84;
(vi)      Kizi – Sitalike – Mpanda (km 95.00): shilingi bilioni 3.00;
(vii)    Mpanda – Mishamo (km 100): shilingi bilioni 1.00;
(viii)  Sumbawanga – Matai – Kasanga (km 112): shilingi bilioni 133.29;

10.      Mheshimiwa Spika,  kwa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, miradi ya barabara inayoendelea ina jumla ya shilingi bilioni 961.072Miradi hiyo ni:-

(i)          Ujenzi wa barabara ya Kimara – Kivukoni (feri), Fire – Kariakoo na Magomeni – Morocco shilingi bilioni 240.90
(ii)        Ujenzi wa karakana na vituo vya mabasi yaendayo kasi (BRT), shilingi bilioni 47.90;
(iii)      Ujenzi wa barabara ya Mwenge – Tegeta, shilingi bilioni 88.00;
(iv)      Kuhamisha miundombinu sehemu ya Mwenge- Morocco, shilingi bilioni 13.801;
(v)        Barabara ya Kilwa (kilwa Road) (km 1.5), shilingi  bilioni 5.46;
(vi)      Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, shilingi bilioni 214.64;
(vii)    Ujenzi wa Flyover TAZARA, shilingi bilioni 60.00
(viii)  Ujenzi wa Barabara ya Gerezani (Gerezani Road) (Bendera Tatu – KAMATA), shilingi bilioni 6.60;
(ix)      Barabara za pete (ring roads) zinazoendelea kujengwa (Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Twiga/ Msimbazi Junction), shilingi bilioni 19.08;
(x)        Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) (Rangi Tatu – Zakhem, awamu ya kwanza (Mradi wa Kajima) shilingi bilioni 29.70;
(xi)      Barabara ya Mandela, shilingi bilioni 61.25
(xii)    Usafiri wa vivuko/boti kati ya Dar es Salaam – Bagamoyo, shilingi bilioni 3.50;




(xiii)  Jet Corner – Vituka – Davis Corner (km 10.30): shilingi bilioni 12.474
(xiv)  Barabara ya Ndundu – Somanga (km 60): shilingi bilioni 58.82;
(xv)    Barabara ya kwenda Uwanja wa Ndege Mafia (km14): shilingi bilioni 2.90
(xvi)  Daraja la Ruvu: shilingi bilioni 0.289
(xvii)Mradi wa ujenzi wa barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata, shilingi bilioni 89.61;
(xviii)  Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km 14): shilingi bilioni 1.75;
(xix)  Barabara zilizokasimiwa Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS,shilingi bilioni 4.398.
Barabara hizo ni :- Shekilango, United Nations, Kifuru – Pugu Stesheni (Mnadani), Kimara – Kinyerezi (Kimara Mwisho), Kawe – TPDF Firing Range – Jangwani, Korogwe – Kilungule – External, Mlimani City – Ardhi – Makongo – Goba, KigogoRound About – Jangwani, Ununio – Buza – Kilungure – Nzasa, Chang’ombe (Makutano ya Kawawa / Nyerere – Polisi Chan’gombe), Taifa Road, Mgulani Road (DUCE – Mgulani JKT), Kinondoni Road, Shaurimoyo Road na Uhuru (Railway Station – Buguruni (Mandela Road).

11.      Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mikoa ya Mwanza na Mara, baada ya barabara za Mwanza – Nyanguge, Mwanza – Ilula na Mwanza – Usagara – Geita kukamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, miradi inayoendelea kwa sasa ina jumla ya shilingi bilioni 100.761Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Makutano – Natta – Mugumu (km 100): shilingi bilioni 3.00;
(ii)        Mwanza / Mara Border – Musoma (km 85.50): shilingi bilioni 85.368
(iii)      Nyanguge – Mwanza/Mara Border (km 85.50): shilingi  bilioni 6.00;
(iv)      Kisesa – Usagara Bypass (km 17.00): shilingi bilioni 1.50
(v)        Nyamswa – Bunda – Kisorya (km 118): shilingi bilioni 1.90
(vi)      Mwanza – Mwanza/Shinyanga Border (km 120): shilingi bilioni 0.55
(vii)    Daraja la Maligisu: shilingi bilioni 1.00
(viii)  Daraja la Kirumi: shilingi bilioni 0.289
(ix)      Geita – Usagara (km 90): shilingi bilioni 1.154

12.      Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kujengwa kwa barabara ya Ilula – Shinyanga – Tinde/Isaka hadi Nzega kwa kiwango cha lami, kwa upande wa Mikoa ya Shinyanga na Simiyu, miradi  ya barabara za lami, kwa sasa ina thamani ya shilingi bilioni 214.14Miradi husika ni pamoja na:-

(i)          Bariadi – Lamadi (km 71.80): shilingi bilioni 67.41
(ii)        Isaka – Ushirombo (km 132): shilingi bilioni 145.34;
(iii)      Kahama Mjini (km 5): shilingi bilioni 0.760
(iv)      Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala Oldeani (km 328) (FS & DD): shilingi bilioni 0.63


13.      Mheshimiwa Spika,  kwa Mikoa ya Dodoma na Singida, miradi iliyokamilika kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Shelui – Singida, Singida – Isuna, Manyoni – Isuna na Dodoma – Manyoni hivyo miradi inayoendelea na inayotegemewa kujengwa kwa kiwango cha lami ina  gharama ya shilingi bilioni 424.4128. Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Dodoma – Manyoni (km 127): shilingi bilioni 0.2308
(ii)        Manyoni – Isuna (km 54): shilingi bilioni 0.577;
(iii)      Dodoma University Road (km 12): shilingi bilioni 0.577
(iv)      Singida – Kateshi (km 65.1): shilingi bilioni 51.63
(v)        Dodoma – Mayamaya (km 43.60): shilingi bilioni 40.61
(vi)      Mayamaya – Bonga (km 188.15): shilingi bilioni 263.958
(vii)    Fufu Escarpment – Dodoma (km 70.90): shilingi bilioni 64.33
(viii)  Daraja la Sibiti: shilingi bilioni 2.50

14.      Mheshimiwa Spika, kwa Mikoa ya Arusha na Manyara, miradi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mikoa hiyo ina jumla ya shilingi bilioni 328.235Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Bonga – Babati (km 19.20): shilingi bilioni 19.69
(ii)        Kateshi – Dareda (km 73.80): shilingi bilioni 64.14
(iii)      Dareda – Babati – Minjingu (km 84.60): shilingi bilioni 84.92
(iv)      Minjingu – Arusha (km 104): shilingi bilioni 75.51
(v)        Arusha – Namanga (km 105): shilingi bilioni 81.77
(vi)      KIA – Mererani (km 23): shilingi bilioni 2.205.

15.      Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya barabara katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga ina jumla ya shilingi bilioni 515.429. Miradi hiyo ni:-

(i)          Korogwe – Handeni (km 65): shilingi bilioni 63.20;
(ii)        Handeni – Mkata (km 54): shilingi bilioni 57.34;
(iii)      Tanga – Horohoro (km 65): shilingi bilioni 69.894;
(iv)      Korogwe – Mkumbara (km 76): shilingi bilioni 62.87
(v)        Mkumbara – Same (km 96): shilingi bilioni 65.13
(vi)      Chalinze – Segera – Tanga (km 245): shilingi bilioni 109.884
(vii)    Rombo Mkuu – Tarakea (km 32): shilingi bilioni 15.80
(viii)  Marangu – Rombo Mkuu na Kilacha – Mwika (km 34): shilingi bilioni 25.10;
(ix)      Kwa Sadala – Masama (km 12.5): shilingi bilioni 5.34
(x)        Kibosho Shine – Kwa Rafael – International School (km 43.00): shilingi bilioni 8.93
(xi)      Rau Madukani – Mawela – Uru Njari (km 12.50): shilingi bilioni 4.88;
(xii)    Kirua Nduoni – Marangu Mtoni (km 31.5): shilingi bilioni 9.10
(xiii)  Sanya Juu – Kamwanga – Bomang’ombe (km 75): shilingi bilioni 7.854;
(xiv)  Same – Himo – Marangu & Mombo – Lushoto (km 132) (Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina): shilingi bilioni 7.854
(xv)    Tanga – Saadani – Bagamoyo (km 178) – Usanifu: shilingi bilioni 2.253

16.      Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Kagera na Geita, miradi inayoendelea kujengwa na ile iliyokamilika ambayo imepangiwa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13 ina thamani ya shilingi bilioni 375.688Miradi hiyo ni pamoja na:-

(i)          Geita – Sengerema (km 90): shilingi bilioni 1.154;
(ii)        Kagoma – Lusahunga (km 154): shilingi bilioni 191.46;
(iii)      Ushirombo – Lusahunga (km 110): shilingi bilioni 114.56
(iv)      Kyaka – Bugene (km 59.10): shilingi bilioni 64.96;
(v)        Uyovu – Biharamulo (km 112): shilingi bilioni 2.40;
(vi)      Kyamyiorwa – Buzirayombo (km 120): shilingi bilioni 0.577;
(vii)    Buzirayombo – Geita (km 100): shilingi bilioni 0.577;

17.      Mheshimiwa Spika, kwa Mikoa ya Lindi na Morogoro barabara ya Somanga – Nangurukuru- Lindi hadi Mingoyo ilikwishakamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Miradi inayoendelea ina thamani ya shilingi bilioni 149.7169 na inajumuisha miradi ya:-
                                                               
(i)          Nangurukuru – Mbwemkulu (km 95): shilingi  bilioni 1.154;
(ii)        Mbwemkulu – Mingoyo (km 95): shilingi bilioni 1.154;
(iii)      Dumila – Rudewa (km 45): shilingi bilioni 41.93;
(iv)      Magole – Turiani (km 48): shilingi bilioni 48.90
(v)        Turiani – Mziha (km 36.6): shilingi bilioni 0.05
(vi)      Daraja la Kilombero: shilingi bilioni 55.00
(vii)    Kidatu – Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha (km 396) (Upembuzi yakinifu na usanifu): shilingi bilioni 1.5289

18.      Mheshimiwa Spika, kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa, miradi inayoendelea ina jumla ya shilingi bilioni 422.493. Miradi hiyo inajumuisha:-

(i)          Ibanda – Itungi Port (km 26): shilingi bilioni 0.657;
(ii)        Msimba – Ruaha Mbuyuni/Ikokoto – Mafinga (km 149.6): shilingi bilioni 127.70
(iii)      Iringa – Mafinga (km 69.4): shilingi  bilioni 64.873
(iv)      Rujewa – Madibira – Mafinga (km 152): shilingi bilioni 0.879;
(v)        Mbeya – Lwanjilo (km 36): shilingi bilioni 27.464
(vi)      Lwanjilo – Chunya (km 36): shilingi bilioni 40.28
(vii)    Chunya – Makongolosi (km 43): shilingi bilioni 1.200
(viii)  Iringa – Migori (km 95.10): shilingi bilioni 84.22
(ix)      Migori – Fufu Escarpment (km 93.80): shilingi bilioni 73.61
(x)        Njombe – Ndulamo – Makete (km 109.4): shilingi bilioni 1.610

19.      Mheshimiwa Spika, gharama za usimamizi wa miradi yote ya barabara na madaraja yanayojengwa katika nchi nzima nishilingi bilioni 170.0.

20.      Mheshimiwa Spika,  miradi ya upembuzi yakinifu na usanifu  wa kina kwa barabara na madaraja inayoendelea katika nchi nzima ina thamani ya shilingi bilioni 6.612 ambazo zinagharamiwa na Mfuko wa Barabara.

21.      Mheshimiwa Spika, miradi ya vivuko iko katika mikoa ya Geita, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Morogoro, Tanga na Pwani. Miradi hii ina jumla ya shilingi bilioni 28.068.

22.      Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya Majengo na nyumba za Serikali katika mikoa yote ya Tanzania inayoendelea ina gharama ya shilingi bilioni 101.932.




23.      Mheshimiwa Spika, ukichukua miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa yote, ikajumuishwa na miradi ya nyumba na vivuko pamoja na miradi ya ukarabati na kazi za matengenezo maalum na ya dharura katika mikoa yote ya Tanzania Bara, miradi iliyo chini ya wizara ya ujenzi kwa ujumla inategemea kuajiri zaidi ya watu 650,000. Idadi hii ni mbali na mama/baba lishe, wachimba kokoto, wafyatua matofali, watengeneza mbao za ujenzi, wachimba mchanga n.k. Wafanyakazi hawa wote watafanya kazi katika miradi niliyoitaja katika mwaka wa fedha wa 2012/13.

24.      Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bodi za CRB, ERB na AQSRB, Bodi ya CRB imekwishasajili Makandarasi wa madaraja yote 9,041 na imewafutia usajili makandarasi 2,576; ERB imesajili Wahandisi 11,264 na imewafutia usajili Wahandisi Washauri 6 na kampuni 5 za ushauri wa kihandisi kwa makosa mbali mbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili na AQSRB imesajili wataalamu wa fani za uwabunifu majenzi na wakadiriaji majenzi 548 na kusajili kampuni 269 za ushauri katika fani hizi.

25.      Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bodi ya Mfuko wa Barabara katika mwaka wa 2012/13 itakusanya shilingi bilioni 400zitakazotumika katika matengenezo ya Barabara na Madaraja yaliyo chini ya Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS na Barabara na Madaraja yaliyo chini ya TAMISEMI.

26.      Mheshimiwa Spika, masuala mengine mtambuka yatakayoshughulikiwa na Wizara ni pamoja na masuala ya Usalama barabarani yaliyotengewa jumla ya shilingi bilioni 4.30288, masuala ya NCC, Utawala, ushirikishwaji wanawake katika kazi za barabara, Chuo cha Morogoro na Mbeya, Mazingira, UKIMWI na usimamizi wa sera na Sheria za nchi na hasa Sheria Na 13 ya mwaka 2007 inayohusu utunzaji wa Barabara.


27.      Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa miradi hii kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 hususani kwa upande wa barabara, Wizara imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kushusha gharama za ujenzi. Hapo awali gharama za ujenzi zilikua zimefikia kiasi cha shs. Bilioni 1.8 kwa km 1, gharama hizi zimeshuka hadi kiasi cha kati ya shs. Milioni 680 hadi 780 kwa km 1. Mfano ni gharama za Ujenzi kwa barabara ya Dodoma – Iringa na Same – Mkumbara. Aidha, jitihada za kutumia Makandarasi wa ndani nazo zimeanza kuzaa matunda kwa makandarasi hao kuanza kuchukua miradi mikubwa ya ujenzi kama ambavyo imetokea katika daraja la Mbutu katika Mkoa wa Tabora wilayani Igunga linalojengwa na muungano wa Makandarasi 13 wazalendo kwa gharama ya shillingi bilioni 12.34.

28.      Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la madeni ya makandarasi. Hivi karibuni Serikali imetoa kiasi cha shillingi Bilioni 300 kwa ajili ya kulipa madeni ya makandarasi. Serikali itaendelea kulipa makandarasi wote kutokana na “certificate” ambazo wanawasilisha kwa kazi wanazofanya. Makandarasi ambao watazembea kazi hawataweza kutengeneza “certificate” na hivyo hawatalipwa. Napenda kutoa wito kwa makandarasi wote nchini kuwa hakuna malipo bila kazi (no certificate no pay).

29.      Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa miradi hii, Wizara imeendelea kuzingatia Sheria mbalimbali hususani Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 26 (Kifungu cha 1 na 2), inatutaka wananchi wote kufuata na kutii Katiba na sheria za nchi. Kwa mantiki hii, inashangaza sana pale Wizara inapoombwa kulipa fidia wananchi ambao kwa mujibu wa sheria wamo ndani ya hifadhi ya barabara. Baadhi ya maombi hayo yanatoka kwetu sisi Viongozi ikiwa ni pamoja na kwenu Waheshimiwa wabunge mliopitisha Sheria Na. 13 ya Mwaka 2007. Kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ambazo ndizo zinatuongoza. Wizara itaendelea kuzingatia sheria na wananchi wote walio ndani ya eneo la hifadhi ya barabara na wale waliokwisha ondolewa hawatalipwa fidia. Kwa wananchi ambao bado wapo ndani ya hifadhi ya barabara wanatakiwa waondoke wenyewe bila fidia. Mameneja wote wa TANROADS mikoani waendelee kusimamia na kuzingatia Sheria, mameneja ambao watashindwa kusimamia sheria kikamilifu na hasa Sheria ya hifadhi ya barabara wataondolewa katika nafasi zao.

VIVUKO NA MAGARI YA SERIKALI

30.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/12 Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imekamilisha ujenzi wa vivuko vipya vya Rusumo, MV Ujenzi (Rugezi – Kisorya) na MV Musoma (Musoma – Kinesi). Wizara kupitia TEMESA inaendelea kukamilisha ujenzi wa vivuko vipya vya Msangamkuu na Kilambo. Aidha, taratibu za ununuzi wa kivuko kipya cha Ilagala zinaendelea na mwezi Mei, 2012 Mkataba ulisainiwa. TEMESA pia imekalilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko cha Rusumo na cha Rugezi – Kisorya (upande wa Kisorya).  Ujenzi wa maegesho ya vivuko vya Chato (Nkome), Rugezi – Kisorya upande wa Rugezi na Bugolora – Ukara unaendelea. Mkandarasi wa kukarabati maegesho ya kivuko cha Kilombero amepatikana na ataanza kazi baada ya kina cha maji kupungua. Mkandarasi wa ujenzi wa maegesho ya Msangamkuu pia amepatikana na ataanza kazi wakati wowote kuanzia sasa.

31.      Mheshimiwa Spika, Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kupitia makusanyo yake ya ndani ya vivuko ya mwaka 2011/12 imeweza kuvifanyia ukarabati vivuko vya MV Nyerere na MV Ukara. Aidha, Wakala umevifanyia matengenezo ya kawaida vivuko vyake 19 vilivyoko nchi nzima. Mwaka 2011/12 Wakala ulipanga kukusanya kiasi cha  shilingi  bilioni 5.00 baada ya kuongeza viwango vya nauli za vivuko Wakala umeweza kukusanya jumla ya shilingi 7,833,585,005.00 hadi Mei 2012. Baada ya kutoa gharama za uendeshaji, shilingi milioni 1,568.781 zimetengwa kununua kivuko/boti nyingine ya Dar es Salaam - Bagamoyo kwa ajili ya kupunguza msongamano Dar-es-Salaam.



UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SERIKALI

32.      Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/12, Wakala wa Majengo Tanzania (Tanzania Buildings Agency - TBA) umeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi; (i) Kutoa huduma ya Ushauri kwa miradi ya ujenzi wa majengo ya Serikali na nyumba za kuishi watumishi wa umma, (ii) Kujenga nyumba za kuwapangisha na kuwakopesha watumishi wa umma, (iii) Kupangisha baadhi ya majengo na nyumba za Serikali kibiashara. Idadi ya nyumba na majengo yaliyo chini ya miliki ya Wakala hadi sasa ni 2,713. Kati ya nyumba hizo, nyumba 1,353 zinapangishwa kibiashara, nyumba 748 zinapangishwa watumishi wa umma, 416 ni za viongozi, 103 nyumba za wageni (Rest Houses), 37 Ikulu ndogo (State Lodges) na 56 ni majengo ya Ofisi, Maghala na Karakana.

33.      Mheshimiwa Spika, taarifa ya mapato yanayotokana na mauzo ya nyumba kwa watumishi wa Serikali, miradi inayoendelea ya nyumba za kibiashara, nyumba za kuwauzia watumishi wa umma na Nyumba za Viongozi wa Serikali (ambazo hazitauzwa -"Tied Quarters") zimeelezwa kwa kina katika Kitabu cha Hotuba yangu ambacho kimesambazwa kwa Waheshimiwa Wabunge.

C:   MAKADIRIO YA  MAPATO  NA  MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2012/2013

34.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Wizara imetengewa jumla ya shilingi 329,085,354,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida.  Kati ya fedha hizo, shilingi 300,764,800,000 ni fedha za Mfuko wa Barabara, shilingi 21,340,508,000 ni fedha za mishahara kwa Wizara na Taasisi na shilingi 6,980,046,000 ni fedha za matumizi mengineyo. Aidha, wizara inakadiria kukusanya jumla ya shillingi15,628,580.





MAKADIRIO YA BAJETI YA MAENDELEO KWA MWAKA  2012/2013

35.      Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka 2012/2013, Wizara imezingatia vipaumbele vya Miradi inayoendelea kutekelezwa, Miradi inayofadhiliwa na wahisani na yenye kuhitaji mchango wa Serikali, Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na  Utekelezaji wa Ahadi za Viongozi Wakuu wa Serikali.

36.          Mheshimiwa Spika, Nchi ya Tanzania ina ukubwa wa eneo linalofikia kilometa za mraba 949,000 na mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 87,581. Mchanganuo wake ni kwamba, km 12,786 ni za Barabara Kuu,  kilometa 22,214 ni za Barabara za Mikoa na Barabara za Wilaya ni kilometa 52,581. Aidha, kuna jumla ya Madaraja 4,880 katika  Barabara Kuu na za Mikoa.


37.    Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013 Wizara ya Ujenzi imetengewa kiasi cha shilingi 693,948,272,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo fedha za ndani ni shilingi 296,896,892,000 na fedha za nje ni shilingi 397,051,380,000.Mgawanyo wa fedha za maendeleo pamoja na miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka 2012/2013 ni kama inavyooneshwa katikaKiambatisho Na.1. Maelezo ya kila mradi ni kama ifuatavyo: -

38.    Mheshimiwa Spika, barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata (Km 107) zimetengwa Shilingi  Milioni 7,396.806 ambapo kati ya fedha hizo milioni 288.55 ni kwa ajili ya kuendelea na usanifu wa barabara ya Bagamoyo – Sadani – Tanga (km 178).

Kwa upande wa barabara ya Usagara – Geita – Kyamyorwa (Km 422) sehemu ya Uyovu – Biharamulo (Km 112) Shilingi Milioni 4,708.40 zimetengwa.





39.    Mheshimiwa Spika, barabara ya Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua - Tabora (Km 443) zimetengwa Shilingi Milioni 30,160.178. Jumla ya shilingi milioni 1,385.093 fedha za ndani na shilingi milioni 6,693.00 fedha za nje zimetengwa ili kuendelea na ujenzi wa lami barabara ya Kidahwe –Uvinza (km 76.6). Kiasi cha shilingi milioni 2,039.70 fedha za ndani  na shilingi milioni 6,130.0 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa daraja la Malagarasi (Daraja la Kikwete). Kiasi cha shilingi milioni 4,767.255 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa barabara ya Tabora - Ndono (km 42) na shilingi milioni 5,645.13  kwa sehemu ya Ndono – Urambo (km 52).  Kwa upande wa barabara ya Tabora – Sikonge (km 70) na barabara ya Ilunde– Kaliua-Urambo (km 146)  kiasi cha shilingi milioni 3,500.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.


40.    Mheshimiwa Spika, barabara ya Marangu – Tarakea – Kamwanga/ Bomang’ombe – Sanya Juu (Km 173) na Arusha – Moshi – Holili (Km 140) zimetengwa Shilingi Milioni 7,854.406 ambapo jumla ya shilingi milioni 488.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu malipo ya mwisho ya mkandarasi wa Tarakea – Rombo na shilingi milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha km 6 za lami kwa barabara ya Marangu – Rombo Mkuu na Mwika Kilacha (km 34). Aidha, kiasi cha shilingi milioni 2,926.00 kimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Sanya Juu – Kamwanga (km 75). Kiasi cha shilingi milioni 1,366 fedha za ndani zimetengwa kuanza ukarabati wa sehemu ya Arusha – Moshi – Holili kwa kiwango cha lami wakati shilingi milioni 28.90 fedha za ndani na shilingi milioni 900.00 fedha za nje zimetengwa kufanya usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Same – Himo na Mombo - Lushoto.

41.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Nangurukuru - Mbwemkulu (Km 95) – Shilingi Milioni 1,154.20 zimetengwa kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho kwa  Mkandarasi. Aidha, kwa barabara ya Mbwemkulu – Mingoyo (Km 95) zimetengwa Shilingi Milioni 1,154.20 ambazo pia ni kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho ya mkandarasi.

42.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Dodoma – Manyoni (KM 127) zimetengwa Shilingi Milioni 230.84 kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi. Aidha, barabara ya Manyoni – Singida (Manyoni – Isuna (Km 54) zimetengwa Shilingi Milioni 577.10 ambazo ni fedha za ndani kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho kwa mkandarasi.

43.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Dumila – Kilosa (Km 78) zimetengwa Shilingi     Milioni 4,767.25 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi. Wakati barabara ya Sumbawanga – Kasesya/Matai - Kasanga Port (Km 112) Shilingi Milioni 7,303.34 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kutumia bajeti ya maendeleo. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu ya barabara ya Matai - Kasesya yenye urefu wa km 46.82 itafanyika.
44.      Mheshimiwa Spika, ujenzi wa madaraja ya Nangoo, Kilombero, Maligisu, Kavuu,  Mbutu, Ruhekei na ununuzi wa madaraja ya chuma kwa ajili ya dharura (Bailey Emergency Bridge) Shilingi Milioni 9,963.62 zimetengwa katika mwaka 2012/2013. Kiasi cha shilingi milioni 577.62 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Daraja la Nangoo, Daraja la Maligisu shilingi milioni 1,000.00, Daraja la Kilombero shilingi milioni 3,028.00, Daraja la Kavuu limetengewa shilingi milioni 1,000.00, Daraja la Sibiti limetengewa shilingi milioni 2,500.00,  Daraja la Mbutu  limetengewa shilingi milioni 300.00, na Daraja la Ruhekei shilingi milioni 577.00. Aidha, shilingi milioni 346.00 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa Bailey Compact Emergency Bridges na crane lorry na shilingi milioni 346.00 zimetengwa kwa ajili ya usanifu wa Daraja la Ruhuhu. Ujenzi wa Daraja la Kirumi umetengewa shilingi milioni 289.00.

45.      Mheshimiwa Spika, barabara ya New Bagamoyo (Kawawa Jct - Tegeta Km 17) zimetengwa Shilingi  Milioni 55,661.324.Lengo la mradi huu ni kupanua barabara hii kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne kuanzia makutano ya Kawawa na Ali Hassan Mwinyi hadi Tegeta ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara hii. Mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la JICA. Jumla ya shilingi milioni 13,801.324 fedha za ndani na shilingi milioni 41,860.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, kulipa fidia na kuhamisha huduma za jamii kwenye eneo la ujenzi (mabomba ya maji, nguzo na nyaya za umeme/simu n.k) katika mwaka 2012/2013.

46.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (Km 178) fedha zilizotengwa ni Shilingi Milioni 4,572.17. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Bugene – kasulo yenye urefu wa km 124 itafanyika. Kwa upande wa barabara ya Isaka – Lusahunga – Rusumo (Km 242) na Nyakasanza - Kobelo (Km 150),  Shilingi Milioni 15,860.20 zimetengwa.Ambapo shilingi milioni 8,779.00 zitatumika kwa sehemu ya Isaka – Ushirombo na shilingi milioni 5,852.20 kwa sehemu ya Ushirombo – Lusahunga kwa ajili ya kuendelea na ukarabati. Aidha, shilingi milioni 29.00 za ndani na shilingi milioni 1,200.00 za nje zimetengwa kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina kwa sehemu ya Lusahunga – Rusumo na Nyakasanza – Kobelo. 

47.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Manyoni – Itigi – Tabora  (Km 254) jumla ya Shilingi      Milioni 16,584.00 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2012/2013. Jumla ya shilingi milioni 8,000.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Tabora – Nyahua na shilingi milioni 8,584.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Manyoni – Itigi – Chaya.

48.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Korogwe – Handeni (Km 65) – Shilingi Milioni 4,779.55 zimetengwa  kwa ajili ya kuendelea na kazi  za ujenzi katika bajeti ya mwaka 2012/2013. Aidha, kwa barabara ya Handeni – Mkata (Km 54) – Shilingi Milioni 4,213.04 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.

49.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwanza/Shinyanga Border – Mwanza (Km 120) – Shilingi Milioni 50.00 zimetengwa.Lengo la mradi huu ni kufanyia ukarabati kwa kiwango cha lami sehemu zilizoharibika za barabara ya mpaka wa Mwanza/Shinyanga – Mwanza. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, jumla ya shilingi milioni 50.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Kwa upande wa barabara ya Mwandiga – Manyovu (Km 60) – Shilingi Milioni 865.65 zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo ya mwisho kwa mkandarasi katika bajeti ya mwaka 2012/2013.

Kuhusu daraja la Umoja, Shilingi Milioni 294.32 zimetengwa kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi.

50.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Ndundu – Somanga (Km 60) zimetengwa Shilingi Milioni 4,077.25. Aidha, barabara ya Kidatu - Ifakara - Lupilo - Malinyi - Londo - Lumecha/Songea (Km 396) Shilingi Milioni 1,528.94 zimetengwa kwa ajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika bajeti ya mwaka 2012/2013.

51.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Tabora - Ipole - Koga – Mpanda (Km 359) - Shilingi Milioni 1,200.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami katika mwaka 2012/2013 kwa sehemu ya Ipole – Koga – Mpanda yenye urefu wa kilometa 273.

Kwa barabara ya Makutano - Natta – Mugumu/ Loliondo – Mto wa Mbu (Km 328) Shilingi Milioni 3,827.96 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Makutano - Natta – Mugumu (km 80) na shilingi milioni 827.96 kwa sehemu ya Mto wa Mbu - Loliondo. Aidha, matatizo ya barabara katika eneo la Mto wa Mbu yatashughulikiwa.






52.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Ibanda – Itungi Port (Km 26) – Shilingi Milioni 657.00 zimetengwa. Aidha, barabara ya Tanga - Horohoro (Km 65) – Shilingi  Milioni 12.00 zimetengwa kukamilisha mradi huu.

53.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Nzega – Tabora (Km 115) imetengewa Shilingi Milioni 10,000.00 ambapo kiasi cha shilingi milioni 5,000.00 kimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa sehemu ya Nzega – Puge na shilingi milioni 5,000.00 kwa sehemu ya Puge – Tabora.

Aidha, barabara ya Sumbawanga – Mpanda - Nyakanazi (Km 829) Shilingi  Milioni  16,800.00 zimetengwa ambapo jumla ya shilingi milioni 6,400.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na kazi ya ujenzi kwa sehemu za Sumbawanga –Kanazi na shilingi milioni 6,400.00 kwa sehemu ya Kanazi – Kizi – Kibaoni. Kiasi cha shilingi milioni 3,000.00 kimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Kizi – Sitalike – Mpanda na shilingi milioni 1,000.00 kimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa sehemu ya  Mpanda – Mishamo (km 100).

54.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyanguge – Musoma  (Km 85.5) na mchepuo wa Usagara - Kisesa (Km 17) zimetengwaShilingi Milioni 7,500.00 ambapo shilingi milioni 6,000.00 kwa ajili ya kuendelea na kazi ya ukarabati wa barabara ya Nyanguge - Musoma. Kiasi cha shilingi milioni 1,500.00 kimetengwa kwa sehemu ya barabara ya Kisesa – Usagara Bypass kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami.

55.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Magole – Mziha (Magole – Turiani (Km 48.8)) zimetengwa Shilingi Milioni 4,110.00 katika bajeti ya mwaka 2012/2013. Katika barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi (Km 171) (Bariadi-Lamadi (Km 71.8)) Shilingi Milioni 7,000.00 zimetengwa.

Aidha, kwa barabara ya Tabora – Ipole – Rungwa (Km 95)  – Shilingi  Milioni 288.55 zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

56.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (Km 310) imetengewa Shilingi Milioni 3,500.00katika Mwaka wa fedha 2012/2013. Lengo la mradi huu ni kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami.

57.      Mheshimiwa Spika, barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Mafia (Mafia Airport Access Road) (Km 14) –  Shilingi Milioni 2,904.85 zimetengwa katika bajeti ya 2012/2013. Lengo la mradi huu ni kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami ili kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na Shirika la Misaada la Marekani (MCC) ambao wametoa fedha za ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mafia kwa makubaliano ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami.

58.      Mheshimiwa Spika, barabara ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (Dodoma University Road) (Km 12)  Shilingi Milioni577.10 zimetengwa. Lengo la mradi huu ni kujenga barabara ya Dodoma – Chuo Kikuu cha Dodoma (km 12) kwa kiwango cha lami. Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Tanzania.

59.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Tunduma – Sumbawanga (Km 231) – Shilingi Milioni 57.88 zimetengwa. Aidha, kwa barabara ya Kagoma – Lusahunga (Km 154) – Shilingi Milioni 10,705.01 zimetengwa. Kazi za ujenzi zilianza Septemba 2009 na zinaendelea.

Kwa upande wa barabara ya Arusha – Namanga (Km 105) - Shilingi Milioni  32,608.89 zimetengwa. Lengo la mradi ni kukarabati barabara hii kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi  milioni 797.89 fedha za ndani na shilingi milioni 31,811.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha ukarabati katika mwaka wa fedha 2012/2013.

60.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Singida - Babati – Minjingu - Arusha (Km 321) Shilingi  Milioni 29, 717.56 zimepangwakatika bajeti ya mwaka 2012/2013 kiasi cha shilingi milioni 240.56 fedha za ndani na shilingi milioni 1,340.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Singida – Katesh; shilingi milioni 336.00 fedha za ndani na shilingi milioni 1,490.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Katesh – Dareda na shilingi milioni 375.00 fedha za ndani na shilingi milioni 2,330.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Dareda – Babati – Minjingu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa sehemu zote tatu. Aidha, kiasi cha shilingi milioni 289.00 fedha za ndani na shilingi milioni 23,317.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza ukarabati wa barabara ya Minjingu - Arusha.

61.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Msimba – Ruaha/Ikokoto - Mafinga (Km  219)  Shilingi  Milioni 18,425.78 zimetengwa ambapo shilingi milioni 3,584.00 fedha za ndani na shilingi milioni 13,962.38 za kigeni zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ukarabati wa km 68.90 za Iringa - Mafinga. Aidha, jumla ya shilingi milioni 29.40 fedha za ndani na shilingi milioni 850.00 fedha za kigeni zimetengwa kwa ajili ya usanifu wa barabara ya Mafinga - Igawa yenye urefu wa km 146.

62.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Korogwe – Mkumbara - Same (Km 172) Shilingi Milioni 52,144.71 zimetengwa. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Katika utekelezaji, mradi huu umegawanywa katika sehemu za Korogwe – Mkumbara (km 76)ambapo jumla ya shilingi milioni 72.41 fedha za ndani na shilingi milioni 26,000.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na kazi ya ukarabati wa sehemu hii ya barabara; aidha, Mkumbara – Same (km 96) ambapo jumla ya shilingi milioni 72.30 fedha za ndani na shilingi milioni 26,000.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na kazi ya ukarabati wa sehemu hii ya barabara.

63.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbeya – Makongolosi (Km 115) Shilingi Milioni 9,544.95 zimetengwa. Ujenzi wa barabara hii umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni: Mbeya – Lwanjilo (km 36); Lwanjilo-Chunya (km 36) na Chunya-Makongolosi (km 43). Barabara hii imetengewa kiasi cha shilingi milioni  4,891.33 kwa sehemu ya Mbeya – Lwanjilo; shilingi milioni 3,253.62 kwa sehemu ya Lwanjilo-Chunya na shilingi milioni 1,200.00 kwa sehemu ya Chunya – Makongolosi kwa ajili ya kuendelea na ujenzi katika mwaka 2012/2013. Aidha, shilingi milioni 200.00 zimetengwa ili kukarabati kwa kiwango cha changarawe sehemu ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa.

64.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Chalinze – Segera - Tanga (Km 248) Shilingi Milioni 12,696.34 zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Chalinze-Kitumbi (km 125) na Kitumbi-Segera-Tanga (km 120).

Katika mwaka wa fedha 2012/13, jumla ya Shilingi milioni 3,121.00 fedha za ndani na shilingi milioni 9,575.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ukarabati wa sehemu ya Kitumbi – Segera – Tanga.

65.      Mheshimiwa Spika, daraja la Ruvu limetengewa Shilingi Milioni 288.55 kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho. Aidha, barabara ya Dodoma – Iringa (Km 260) imetengewa Shilingi Milioni 57,930.00. Kiasi cha shilingi milioni 400.00 fedha za ndani na shilingi milioni 20,050 fedha za nje zimetengwa kwa sehemu ya Iringa – Migori; shilingi milioni 350.00 fedha za ndani na shilingi milioni 17,550 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Migori – Fufu Escapment na shilingi milioni 380.00 fedha za ndani na shilingi milioni 19,200 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Fufu Escapment – Dodoma kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.

66.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Dodoma – Babati (Km 261) zimetengwa Shilingi Milioni 36,875.91. Utekelezaji wa mradi huu umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni: Dodoma – Mayamaya (km 43), Mayamaya – Mela- Bonga (km199 ) na Bonga – Babati (km 19.20).





Katika mwaka wa fedha 2012/13, kiasi cha shilingi milioni 4,291.91 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Dodoma – Mayamaya na shilingi milioni 2,200.00 fedha za ndani zimetengwa kwa sehemu ya Bonga – Babati.

Sehemu ya Mayamaya – Mela (km 99.35), jumla ya shilingi milioni 577.00 fedha za ndani na shilingi milioni 14,380.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa sehemu hii ya barabara.

Sehemu ya Mela – Bonga (km 88.80), jumla ya shilingi milioni 577.00 fedha za ndani na shilingi milioni 14,850.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa sehemu hii ya barabara.

67.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Masasi- Songea – Mbamba Bay (Km 649) Shilingi Milioni 125,496.85 zimetengwa katika sehemu zifuatazo:- Masasi – Mangaka (km 54), Mangaka – Tunduru (km 137), Mangaka – Mtambaswala (km 65.5), Namtumbo - Kilimasera (km 60.7); Kilimasera – Matemanga (km 68.2), Matemanga – Tunduru (km 58.7), Songea - Namtumbo (km 67), Peramiho – Mbinga (km 78) na Mbinga -  Mbamba Bay (km 66).

Ujenzi wa mradi huu kwa barabara ya Masasi – Mangaka umekamilika.

68.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Peramiho – Mbinga – Mbamba Bay, ujenzi wa sehemu ya Peramiho Junction – Mbinga (km78) unagharamiwa kwa fedha za msaada kutoka Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa MCC na mchango wa Serikali ya Tanzania na kazi za ujenzi zinaendelea.

69.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, zimetengwa jumla ya shilingi milioni 346.85 fedha za ndani na shilingi milioni 7,300 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Mangaka – Nakapanya; shilingi milioni 346.00 fedha za ndani na shilingi milioni 6,500.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Nakapanya – Tunduru; shilingi millioni 346.00 fedha za ndani na shilingi milioni 6,909.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Mangaka – Mtambaswala; shilingi milioni 3,617.00 milioni fedha za ndani na shilingi milioni 33,616.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Tunduru – Matemanga; shilingi milioni 3,040.00 fedha za ndani na shilingi milioni 28,359.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Matemanga – Kilimasera; shilingi milioni 3,040.00 fedha za ndani na shilingi milioni  27,685.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya sehemu ya Kilimasera – Namtumbo; shilingi milioni 17.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya Songea – Namtumbo; shilingi milioni 17.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya Peramiho – Mbinga; shilingi milioni 2,600.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Mbinga – Mbamba Bay; shilingi milioni 29.00 fedha za ndani na shilingi milioni 950.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na usanifu wa sehemu ya Makambako – Songea na shilingi milioni 29.00 fedha za ndani na shilingi milioni 750.00 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na usanifu wa sehemu ya Mtwara – Mingoyo – Masasi.

MIRADI YA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

70.      Mheshimiwa Spika, katika kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, Wizara inaendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 899.063Maelezo zaidi juu ya miradi hii inayotekelezwa kwa Dar es salaam pekee na gharama zake kama nilivyoielezea hapo awali yapo kwenye Kitabu cha Hotuba ya Bajeti yangu.

71.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/13, Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la dar es Salaam kama ifuatavyo:-



Barabara za Pete (Ring Roads)  (km 98.15)

72.          Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2012/2013, kiasi cha shilingi milioni 1,073.00 kimetengwa kwa ajili ya kukamilisha kazi zilizobakia kwa barabara ya Ubungo Bus Terminal –Kigogo-Kawawa Roundabout; shilingi milioni  1,000.00  kwa barabara ya Kawawa Roundabout – Msimbazi Valley –Jangwani/Twiga Junction na shilingi milioni 1,200.00 kwa barabara ya Jet Corner – Vituka – Devis Corner.

Kiasi cha shilingi milioni 577.00 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati barabara ya Ubungo Maziwa – External na Tabata Dampo – Kigogo, shilingi milioni 1,000.00 kimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Kimara – Kilungule – External; shilingi milioni 2,000.00 zimetengwa kwa ajili ya barabara ya Mbezi (Morogoro Road) –Malambamawili (pamoja na barabara iendayo Shule ya Msingi Malambamawili (km2) – Kinyerezi – Banana; shilingi milioni 2,100.00 kwa ajili ya barabara ya Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi (Morogoro Road); shilingi milioni 1,000.00 kwa ajili ya barabara ya Tanki Bovu – Goba; shilingi milioni 577.00 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Kimara – Baruti – Msewe – Changanyikeni na shilingi milioni 50.00 zitatumika kufuatilia na kusimamia ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo kwa kasi (Bus Rapid Transit Infrastructure).

Aidha, Wizara kupitia TANROADS itazihudumia barabara ambazo ziko chini ya TANROADS Dar  es Salaam ambapo jumla ya shillingi bilioni 18 zimetengwa. Wizara pia ina mpango wa kujenga Dar es Salaam – Chalinze-Morogoro Express Way kwa utaratibu wa Public Private Partnership (PPP).

73.      Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Flyovers Dar Es Salaam na barabara za maingilio Shilingi Milioni 2,000.00 zimetengwa wakati Daraja la Kigamboni limetengewa  Shilingi Milioni 2,788.55. Aidha, barabara ya Sam Nujoma (Km 4) imetengewa Shilingi Milioni 318.36 kwa ajili ya kulipa sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi.
74.      Mheshimiwa Spika, barabara ya Dar es Salaam – Mbagala (Kilwa Road) (Km 12.9) imetengewa Shilingi Milioni 8,100.00,lengo la mradi huu ni kukarabati na kupanua barabara ya lami kutoka njia mbili hadi nne kati ya Gerezani na Mbagala kwa msaada kutoka Serikali ya Japan na Serikali ya Tanzania. Mradi huu unatekelezwa kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza inahusisha sehemu ya Bendera Tatu – Mtoni kwa Azizi Ally (km 5), awamu ya pili inahusisha sehemu ya Mtoni kwa Azizi Ally – Mbagala Zakhem (km 5.1), awamu ya tatu inahusisha sehemu ya Mbagala Zakhem – Mbagala Rangi Tatu (km 1.5) na awamu ya nne inahusisha upanuzi wa sehemu ya Bendera Tatu – Gerezani (km 1.5). Awamu ya kwanza na ya pili imejengwa kwa msaada wa fedha kutoka Serikali ya Japan.

Mkataba wa awamu ya tatu kwa ajili ya barabara yenye urefu wa km 1.5 ulisainiwa tarehe 19 Oktoba, 2010 na umekamilika Mei, 2012. Mradi huu umegharamiwa na Serikali ya Tanzania.




Katika mwaka wa fedha 2012/13 mradi wa Mbagala Zhakhem – Mbagala Rangi Tatu umetengewa shilingi milioni 1,500.00 kwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo ya kazi hizo. Aidha, kiasi cha shilingi milioni 6,600.00 kimetengwa kwa ajili ya maandalizi ya upanuzi wa sehemu ya Bendera Tatu – Gerezani (KAMATA).

75.      Mheshimiwa Spika, maegesho ya Vivuko Dar Es Salaam – Bagamoyo Shilingi Milioni 2,000.00 zimetengwa wakati Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata (Km 107) – Shilingi milioni 7,396.806. Aidha, barabara zilizokasimiwa Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS (km 78.64) zimetengewa Shilingi bilioni 4.398.

76.      Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Makao Makuu ya Wakala wa Barabara (Tanroads) zimetengwa  Shilingi Milioni  120.50.Aidha, kwa ujenzi wa barabara za Uongozi Institute (Km 8.8) Shilingi Milioni 405.50 zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya mchepuo kutoka barabara ya Bagamoyo kuingia Chuoni pamoja na barabara zilizoko ndani ya Chuo hicho.

BARABARA ZA MIKOA SHILINGI MILIONI 20,410.00

77.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/13, miradi ya maendeleo ya barabara za Mikoa imetengewa jumla ya shilingi milioni  20,410.00 zote zikiwa fedha za ndani. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kufanya ukarabati wa jumla ya km 337.60 kwa kiwango cha changarawe na kujenga km 23.70 kwa kiwango cha lami kwa kutumia fedha za bajeti ya maendeleo. Kazi za ukarabati kwa kiwango cha changarawe zitafanyika katika Mikoa yote. Aidha, ujenzi wa madaraja 14 utatumia fedha za bajeti ya maendeleo katika Mikoa ya Morogoro (2), Mbeya (3), Manyara (1), Mtwara (1), Ruvuma (1), Simiyu (4),  Lindi (1) na Rukwa (1). Orodha ya miradi ya barabara  za  Mikoa kwa  kutumia  fedha  za bajeti ya maendeleo imeoneshwa katika Kiambatisho Na 2.
UJENZI WA MAEGESHO YA VIVUKO - SHILINGI MILIONI 4,800.00

78.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2012/13, Wizara imetenga kiasi cha shilingi milioni 4,800.00  kwa ajili ya ujenzi wa maegesho ya vivuko. Wizara kupitia TEMESA imepanga kuendelea na ujenzi wa maegesho (ramps) katika vivuko vya Msangamkuu (shilingi milioni 478.48), Rugezi-Kisorya (shilingi milioni 111.32) na kulipia sehemu ya gharama ya ujenzi wa maegesho ya Utete (shilingi milioni 954.00). Aidha, Wizara kupitia TEMESA imepanga kuanza ujenzi wa maegesho ya kivuko cha  Maisome-Kahunda (shilingi milioni 400.00), Ruhuhu (shilingi milioni 400.00) na kivuko cha Chato maegesho yake matano ya Muharamba, Kikumbiitale, Bukondo, Senga na Zumacheli (shilingi milioni 456.2).

79.      Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na juhudi za kuanzisha usafiri wa boti/kivuko katika mwambao wa Bahari ya Hindi kuanzia Dar es Salaam hadi Bagamoyo kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Mradi huu utatekelezwa hatua kwa hatua ambapo shilingi milioni 2,000.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa maegesho.

UNUNUZI WA VIVUKO VIPYA NA VIFAA VYA KARAKANA- SHILINGI MILIONI 2,571.149

80.      Mheshimiwa Spika, Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imetenga jumla ya shilingi milioni 2,571.149 kutoka Bajeti ya Maendeleo kwa ajili ya ununuzi wa vivuko vipya.  Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 1,939.050 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa kivuko kipya cha Ilagala (Kigoma) na kiasi cha shilingi milioni 632.099 zimetegwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya karakana za TEMESA.

UKARABATI WA VIVUKO - SHILINGI MILIONI 799.415

81.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka fedha 2012/13, Wizara imetenga kiasi cha shilingi milioni 799.415 kwa ajili ya ukarabati wa vivuko. Wizara kupitia TEMESA imepanga kukarabati vivuko vya MV Chato (shilingi milioni 129.00), MV Geita (shilingi milioni 100.00), MV Kome I (shilingi milioni 100.00), MV Kilombero I (shilingi milioni 180.84), MV Sabasaba (shilingi milioni 250.00) na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi (shilingi milioni 39.575). Ukarabati wa vivuko hivi utaviwezesha viendelee kutoa huduma kwa uhakika na usalama kwa wananchi katika maeneo husika.

UJENZI NA UKARABATI WA NYUMBA NA MAJENGO YA SERIKALI-SHILINGI MILIONI 5,978.772

82.      Mheshimiwa Spika, mradi huu umelenga kujenga nyumba za makazi ya viongozi na watumishi wa Serikali wenye stahili hiyo.

Kipaumbele kwa sasa ni katika ujenzi wa nyumba za Waheshimiwa Majaji pamoja na viongozi wengine wa Serikali wenye stahili ya kupewa nyumba na Serikali.


83.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha  2012/13 jumla ya shilingi milioni 2,364.83 zimetengwa kwa ajili  ya ujenzi wa nyumba za Waheshimiwa Majaji katika Mikoa ya Kilimanjaro (1), Mtwara (1), Kagera (1) na Shinyanga (1) pamoja na umaliziaji wa nyumba za Waheshimiwa Majaji katika Mikoa ya  Tabora (1), Dar es Salaam (2) Mbeya (1), Mwanza (1), Iringa (1), Tanga (1), Dodoma (1), Ruvuma (1) na Arusha (1). Aidha, jumla ya shilingi milioni 475.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za viongozi wa Serikali katika Wilaya za Kasulu (1) na Ilala (1) pamoja na umaliziaji wa nyumba za Viongozi katika Wilaya za Urambo (1), Ukerewe (2), Bahi (2), Kondoa (1) na Mvomero (1). Kiasi cha shilingi milioni 400.00 zimetengwa kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bariadi Mkoani Simiyu.

84.      Mheshimiwa Spika, Wizara imetenga jumla ya shilingi milioni 260.942 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Mwangaza (Dodoma) na zahanati ya Lindi (Manispaa). Miradi mingine iliyotengewa fedha ni pamoja na shilingi milioni 200.00 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za viongozi wa Serikali katika Wilaya ya Siha, shilingi milioni 374.400 kwa ajili ya uhifadhi wa jengo la Boma la Kale Bagamoyo, shilingi milioni 542.00 kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira ya nje na ndani pamoja na ujenzi wa uzio kuzunguka nyumba za viongozi Dar es Salaam. Aidha, ukarabati wa karakana za TEMESA, karakana za uselemara na ofisi za vikosi vya ujenzi zimetengewa shilingi milioni 565.77. Wizara imetenga kiasi cha shilingi milioni 375.83 kwa ajili ya kazi za ushauri, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi. Wizara pia imetenga jumla ya shilingi milioni 420.00 kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ujenzi wa nyumba 10,000 za Watumishi wa serikali katika Mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara. Aidha, katika mwaka wa fedha 2012/2013, Wizara kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), imepanga kujenga nyumba 2,500 katika Mikoa yote Tanzania Bara. Jumla ya shilingi milioni 180,000.00 zitatumika kukamilisha mradi huu. Fedha hizi zitatokana na mkopo ambao TBA wataupata kutoka mabenki ya hapa nchini. Katika hatua za maandalizi, TBA imepata jumla ya viwanja 2,253 katika Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara ikiwemo mikoa mipya minne ya Njombe, Katavi, Simiyu na Geita. Katika mikoa hiyo mipya, Wakala umeahidiwa kupewa jumla ya viwanja 600 kwa mchanganuo wa viwanja 100 Mkoa wa Katavi, viwanja 100 Mkoa wa Njombe, viwanja 100 Mkoa wa Geita na viwanja 300 Mkoa wa Simiyu.

85.      Mheshimiwa Spika, Usalama Barabarani zimetengwa Shilingi Milioni 4,302.88 ambazo zitahusisha kujengwa kwa mzani wa kisasa katika eneo la Vigwaza na kuhamisha mzani wa kibaha. Aidha,  mazingira na marekebisho ya mfumo Shilingi Milioni 800.00zimetengwa wakati Menejimenti ya Utunzaji wa Mazingira zimetengwa Shilingi Milioni 357.00, na Institutional Support Shilingi Milioni 992.472 zimetengwa. Wizara itaendelea kuratibu na kusimamia miradi hii kama ilivyofafanuliwa kwenye Kitabu cha Hotuba yangu ambacho kimesambazwa kwa Waheshimiwa Wabunge.



FEDHA ZA MFUKO WA BARABARA KWA MWAKA 2012/13

86.      Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, kiasi cha shilingi 300,764,800,000.00 fedha za Mfuko wa Barabara zitatumika kwa ajili ya kufanya matengenezo ya barabara; utekelezaji wa miradi mbali mbali ya barabara na vivuko na usimamizi wa utekelezaji wa miradi hiyo. Kati ya fedha hizo Wizara ya Ujenzi imetengewa shilingi 29,775,720,000.00 na TANROADS shilingi 267,981,436,800.00. Aidha, Bodi ya Mfuko wa Barabara imetengewa shilingi 3,007,643,200.00. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 728.848 ni kwa ajili ya mishahara, shilingi milioni 1,091.285 ni kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi ya barabara nchi nzima ikiwamo ile ya Halmashauri za Wilaya, shilingi milioni 192.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Jengo la Ofisi Dodoma na shilingi milioni 995.51 ni kwa ajili ya uendeshaji. 


Fedha za Mfuko wa Barabara zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi zitatumika kutekeleza miradi ifuatayo:-

(i)    miradi ya Barabara za Mikoa ambayo imetengewa shilingi  milioni 15,524.90 kama inavyooneshwa kwenye Kiambatisho Na. 3;
(ii)  miradi ya Barabara Kuu ambayo imetengewa shilingi milioni 9,011.71 kama inavyooneshwa katika Kiambatisho Na. 4;
(iii)          miradi ya vivuko kama ifuatayo: ununuzi wa kivuko kipya cha Maisome-Kahunda (Geita) shilingi milioni 1,159.05, ununuzi wa kivuko kipya cha Itungi Port (Kyela) chenye uwezo wa kubeba tani 50 shilingi milioni 963.74 na ununuzi wa vipuri vya vivuko 19 nchini shilingi milioni 840.95.
(iv)          kazi za dharura za barabara na madaraja pamoja na shughuli za usalama barabarani na mazingira shilingi milioni 1,150.00.






MPANGO WA MATENGENEZO YA BARABARA KWA MWAKA 2012/13

87.      Mheshimiwa Spika, fedha za matengenezo ya Barabara Kuu na Barabara za Mikoa kwa mwaka 2012/13 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara ni jumla ya shilingi 267,981,436,800.00. Maelezo ya jinsi fedha hizi zitakavyotumika yapo katikaViambatisho Na. 5A hadi 5E ya Kitabu cha Hotuba yangu na maelezo zaidi kuhusu mpango wa matengenezo ya barabara waheshimiwa wabunge watayapata humo.

88.      Mheshimiwa Spika, Mpango Maalum wa Kitaifa wa kuinua Matumizi ya Teknolojia ya Nguvu Kazi pamoja na Ushirikishwaji wa Wanawake katika kazi za barabara nchini zimetengwa jumla ya Shilingi Milioni 219.90 (Kutoka Mfuko Wa Barabara)





Aidha, kuhusu Maendeleo ya Watumishi katika Mwaka 2012/2013 watumishi 132 wanatarajiwa kupewa mafunzo, kati ya hao watumishi 29 watahudhuria mafunzo ya muda mrefu ndani ya nchi na watumishi 103 watahudhuria mafunzo ya muda mfupi ndani ya nchi.

Pia wafanyakazi wa muda mfupi na muda mrefu wanaokadiriwa kuwa 650,000 wanatarajiwa kupata ajira katika miradi ya barabara, vivuko na katika miradi ya ujenzi wa nyumba na majengo ya Serikali kwa mchanganuo ufuatao;

89.      Mheshimiwa Spika, Miradi mikubwa zaidi ya 120 inayoendelea nchini na kusimamiwa na Wizara (TANROADS) inategemea kutengeneza ajira ya watu/wafanyakazi 320,000 ikizingatiwa kuwa mkataba wa mradi mmoja huajiri hadi watu 3,000.  Mradi wa kawaida huwa na malori makubwa (tippers) yasiyopungua 40, malori ya kawaida zaidi ya 10, grader, vijiko, bulldozers, excavetor na Rollers zisizopungua 50, crusher, service vihicles na mitambo mbalimbali.  Hutoa ajira za walinzi, madereva, wapishi, mafundi, wachoraji, wahandisi, watafiti wa udongo, watunza stoo, wataalam wa huduma ya kwanza, wataalam wa mikataba, consultants, vibarua, n.k.

90.      Mheshimiwa Spika, miradi midogo inayosimamiwa na TANROADS katika mikoa yote 25 ya Tanzania Bara yenye jumla ya Makandarasi 1,500 huajiri wafanyakazi wasiopungua 50 kwa kila Kandarasi. Shughuli zinazofanyika katika miradi hii midogo ni pamoja na Periodic Maintenance, Spot Improvement, Routine and Emergence Maintenance n.k. Miradi hii inategemea kutengeneza ajira za watu 75,000.

91.      Mheshimiwa Spika, miradi inayosimamiwa na TEMESA, Wakala inayohusika na magari, vivuko, mifumo ya umeme n.k. katika mikoa yote 25 ya Tanzania Bara ikihusisha Makandarasi wakubwa wa kujenga/kukarabati vivuko na maegesho ya vivuko (Ramps) pamoja na miradi mikubwa ya mifumo ya umeme kwenye majengo ya Serikali inategemea kutengeneza ajira za watu 20,000. Aidha ajira ya walinzi katika maeneo mbalimbali itahusika.

92.      Mheshimiwa Spika, miradi inayosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika nchi nzima ambapo inahusisha ujenzi wa miradi mikubwa ya nyumba, walinzi, ushauri (Consultancy) n.k. inategemewa kutengeneza ajira ya watu 25,000.

93.      Mheshimiwa Spika, miradi yote inayosimamiwa na Mfuko wa Barabara (RFB) katika mikoa na Wilaya yote nchini; ikizingatiwa kila Wilaya ina Makandarasi watano tu na kila Kandarasi ameajiri watu 80 (kuchimba mchanga, kulima barabara, kuchimba kokoto kuchimba mitaro, wafagia barabara n.k.).  Kwa idadi ya chini kabisa kila Wilaya itatengeneza ajira za watu 400. Hivyo kwa Wilaya zote 133 unapata ajira za watu zaidi ya 53,000 kutengenezwa kupitia fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund).

94.      Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usajili Makandarasi Tanzania (CRB) imekwishasajili Makandarasi 9,041 walio hai.  Kwa wastani kampuni ili isajiliwe lazima iwe na Mkurugenzi wa Kampuni, Engineer, Magari, Dereva, Walinzi n.k.  Kampuni kubwa huajiri watumishi kati ya 30 – 40 na kampuni ndogo huajiri watumishi 5 – 15.  Tumechukua wastani wa watumishi 15 tu kwa kila kampuni kwa makampuni 9,041, tunatarajia kutengeneza ajira za watu 135,615.

95.      Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) ilikwishasajili Wahandisi 11,264.  Aidha Bodi itasimamia utekelezaji wa mpango wa mafunzo ya vitendo kwa Wahandisi wahitimu 1,000 katika mwaka 2012/13.  Aidha, Kampuni za Ushauri wa Kihandisi zitafika 257 katika mwaka wa fedha 2012/13.  Makampuni ya Kihandisi hutengeneza ajira kati ya watu 15 – 30.  Hivyo Bodi ya ERB inategemea kwa kiwango cha chini kabisa kutengeneza ajira za watu wasiopungua 11,000.

96.      Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usajili wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Wajenzi (AQRB), ilikwishasajili Watalaamu wa fani hii wapatao 548 na hivyo Bodi hii inategemea kutengeneza ajira za watu 3,000.

97.      Mheshimiwa Spika, Baraza la Taifa la Ujenzi (N.C.C), hufanya utafiti mbalimbali kuhusu sekta ya ujenzi.  Aidha, hutoa ushauri na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayohusu sekta ya ujenzi.  Hivyo N.C.C wanategemea kutengeneza ajira ya watu zaidi ya 1,000.

98.      Mheshimiwa Spika, miradi iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi Makao Makuu mfano miradi iliyo chini ya Vikosi vya Ujenzi, Usalama Barabarani, Mazingira, Utawala, Uhasibu, Ukaguzi n.k. itatengeneza ajira za watu wasiopungua 3,000.

Hivyo katika mwaka wa 2012/13 Wizara ya Ujenzi inategemea kutengeneza ajira za watu wasiopungua 650,000.



99.      Mheshimiwa Spika, shughuli mbalimbali zilizopangwa kutekelezwa za Wakala na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ikiwa ni pamoja na Wakala wa Barabara, Wakala wa Majengo ya Serikali, Wakala wa ufundi na Umeme, Bodi ya Mfuko wa Barabara, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Baraza la Taifa la Ujenzi, Vikosi vya Ujenzi, Chuo cha Ujenzi Morogoro na Kituo cha Usambazaji wa Tekinolojia katika Sekta ya Uchukuzi zimefafanuliwa kwa kina katika Kitabu cha Hotuba yangu ambacho kimesambazwa kwa Waheshimiwa wabunge.

SHUKURANI

100. Mheshimiwa Spika, napenda  nitumie fursa hii  kuwashukuru kwa dhati Wabunge wote, nikielekeza shukrani maalum kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa michango, ushauri na ushirikiano waliotupa katika kuimarisha huduma zitolewazo na Wizara. Wizara  inaahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yatakayotolewa na Bunge lako Tukufu wakati wa kujadili bajeti hii.

101. Mheshimiwa Spika, shukurani zetu ziwaendee Washirika wetu wa Maendeleo waliochangia katika kutekeleza programu na mipango yetu ya sekta ambao ni pamoja na Abu Dhabi, Canada (CIDA), Demark (DANIDA), Japan (JICA), Korea, Marekani (MCC), Uingereza (DFID), Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (BADEA), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU), Kuwait Fund na OPEC Fund. Aidha, tunawashukuru wadau wengine mbalimbali hususani wa sekta binafsi, kwa ushiriki wao katika ujenzi wa barabara, madaraja, nyumba na vivuko pamoja na ushirikiano wanaotupa katika kutekeleza malengo ya sekta.


102. Mheshimiwa Spika, ninawashukuru kwa dhati viongozi wenzangu katika Wizara nikianza na Mhe. Eng. Gerson H. Lwenge (Mb.), Naibu Waziri; Balozi Herbert E. Mrango, Katibu Mkuu; Eng. Dkt. John S. Ndunguru, Naibu Katibu Mkuu; Wenyeviti wa Bodi za Mfuko wa Barabara, Usajili wa Makandarasi, Usajili wa Wahandisi, Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Baraza la Taifa la Ujenzi, TANROADS, TEMESA na TBA kwa ushirikiano walionipa. Aidha, ninawashukuru Watendaji Wakuu wa TANROADS, TBA, TEMESA, Mfuko wa Barabara, Bodi za Usajili wa Makandarasi, Usajili wa Wahandisi, Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Baraza la Taifa la Ujenzi, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kunipa katika kipindi cha uongozi wangu. Napenda pia kumshukuru Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), ambaye alikua Naibu Waziri wangu kwa kazi nzuri alizofanya wakati nikiwa naye Wizara ya Ujenzi kabla hajahamishiwa Wizara ya Uchukuzi. Nawashukuru sana.

103. Mheshimiwa Spika, napenda pia niwashukuru kwa dhati wapiga kura wangu wa Jimbo la Chato kwa ushirikiano wao mkubwa wanaonipa katika kuleta maendeleo ya Jimbo letu pamoja na uvumilivu walionao kwangu wakati nikitekeleza majukumu ya kitaifa. Nawashukuru sana.

HITIMISHO

MAKADIRIO YA MATUMIZI YA KAWAIDA 2012/2013

104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13, Wizara ya Ujenzi inaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya shilingi 329,085,354,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, shilingi 21,340,508,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zake, shilingi 300,764,800,000.00 ni fedha za Mfuko wa Barabara na shilingi 6,980,046,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo ya Wizara na Taasisi.


BAJETI YA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2012/13

105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/13, Wizara ya Ujenzi inaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla yashilingi 693,948,272,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi 296,896,892,000.00 ni fedha za ndani na shilingi 397,051,380,000.00 ni fedha za nje.

MUHTASARI WA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI KWA MWAKA 2012/2013

89.          Na.
MAELEZO
KIASI (SHILINGI)
90.           1
Mishahara
21,340,508,000
91.           2
Mfuko wa Barabara
300,764,800,000
92.           3
Matumizi Mengineyo
6,980,046,000
93.            
Jumla ya Fedha za Matumizi ya Kawaida
329,085,354,000
94.           1
Fedha za ndani kwa Miradi ya Maendeleo
296,896,892,000
95.           2
Fedha za nje kwa Miradi ya Maendeleo
397,051,380,000
96.            
Jumla Fedha za Maendeleo
693,948,272,000
97.            
JUMLA KUU
1,023,033,626,000

106.         Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.


DONDOO MUHIMU ZA  HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, MHESHIMIWA DKT.  JOHN  POMBE MAGUFULI  (MB).


  1. Serikali ya Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yaendelea na ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 11,154.35 kwa lami. Magufuli azitaja kwa kila Mkoa.

  1. Jumla ya shilingi bilioni 6,005.63653 kutumika katika ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara, madaraja, vivuko, nyumba na majengo ya Serikali nchini

  1. Ajira 650,000 kutokana na miradi chini ya Wizara ya ujenzi pekee.

  1. Wizara ya ujenzi yaendelea kufutia usajili Makandarasi, Wahandisi na Wahandisi Washauri wasiotekeleza wajibu wao ipasavyo.

  1. Umakini wa magufuli washusha bei ya gharama za ujenzi wa barabara kutoka bilioni 1.8kwa km mwaka 2010 hadi kati ya milioni 680 – 780 kwa km mwaka 2011/2012

  1. Bilioni 300 zatolewa na Serikali ya JK kulipa madeni ya makandarasi

  1. Makandarasi wasiofanya kazi kutolipwa

  1. Magufuli aendelea kukomalia sheria, walioondolewa toka hifadhi ya barabara kutolipwa; waliojenga kuondolewa bila fidia; awapasha wabunge ndio waliotunga sheria.

  1. Ujenzi wa Madaraja ya Kigamboni, Kilombero na Kikwete (Malagarasi) waanza; flyover ya TAZARA nayo yatengewa fedha.

  1. Dar – Chalinze - Mororgoro kuunganishwa na “express way”; mradi wa mabasi yaendayo kasi nao kukamilika kwa wakati.

  1. Tatizo la  Makutano - Natta – Mugumu/ Loliondo – Mto wa Mbu lapatiwa ufumbuzi, kuanza kujengwa kwa lami

  1. Boti kuanza kusafirisha abiria na mizigo kati ya Dar es salaam na  Bagamoyo

  1. Wakala wa majengo kujenga nyumba 2,500 nchi nzima. Viwanja 2,253 Mikoa yote ikiwemo Mikoa mipya vyapatikana.


No comments: