Friday, July 13, 2012

EXCLUSIVE HABARI 4 KUTOKA MTWARA....Na Idrisa Bandali

NALIENDELE
Chuo cha utafiti wa kilimo naliendele wametoa mafunzo kwa mabwana shamba wote wa mikoa inayolima zao la korosho ili kuboresha zao hilo. Kwa usimamizi wa Bodi ya korosho na Mfuko wa  wakfu wa pembejeo.
Akizungumza katika semina hiyo Dr elly kafiriti, mkurugenzi wa chuo cha utafiti wa kilimo naliendele amesema kuwa  pamoja na kuwepo na njia za kuzuia magonjwa katika zao la korosho lakini bado tatizo ni kubwa.
Amesema kuwa wakulima wamekuwa wanapuliza dawa mara moja badala ya kupulizia mara nne (4) kwa msimu mmoja wa zao hilo la korosho .
Kupitia mafunzo hayo ya  mabwana shamba Ndugu kafiriti amesema kuwa wanaimani kubwa ya kuwa wakulkima watafuata utaratibu mzuri wa kupulizia masghamba yao kutoka kwa mabwana shamba hao waliopata mafunzo hayo
Aidha amesema kuwa kwa kuwa hakuna uwian o mzuri kati ya dawa zinazoagizwa na serikali kupitia usimamizi wa halmashaurio husika ndio hupelekea kuwepo kwa tatizo la kupungua kwa pembejeo hizo
Mkurugenzi anasema kuwa kutokana na utafiti uliofanywa wamegundua changamoto mbalimbali katika kufanikisha kuzalishwa kwa zao hilo na ameahidi kuzifanyia kazi
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
UDHIBITI
Uthibiti wa fedha za miradi kutoka serikali kuu na zile zinazo kusanywa na halmashauri kukamilika kwa miradi husika zimesababisha kupata hati safi kwa mwaka 2012-2013.
hayo yamebainishwa katika kikao cha baraza la madiwani na mwenyekiti wa halmasahuri ya wilaya mtwara Ndugu Mussa Ndazigula alipokuwa anafungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbbi wa ttc kawaida mkoani hapa
Amesema kukaguliwa kwa mara kwa mara na wakaguzi wa mahesabu kutazifanya  halmashauri kuwa na umakini katika matumizi mabaya ya fedha za miradi zinazotolewa na serikali kuu na zile zinazo kusanywa na halma shauri husika.
Ndugu Ndazigula amewashukuru madiwani na wakuu wa idara kwa mshikamano walionyesha hadi kufanikisha kupata hati safi mwaka huu
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
NEWALA
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala amefungua mafunzo ya mgambo katika Kata ya Mnyambe Wilayani  Newala, mkoani Mtwara hii leo.

Akihutubia wana mafunzo ya mgambo katika Kata hiyo ya Mnyambe, Mkuu wa Wilaya hiyo amewaasa na kuwafafanulia wana mafunzo kwamba, mafunzo hayo ya mgambo yapo kwa mujibu wa sheria namba 147 ya mwaka 1977 na kwa mjibu wa sheria inayounda jeshi la Wananchi (JWTZ) ya mwaka 1966 na hivyo wapuuze upotoshwaji unaotolewa na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakieneza uvumi kwamba mgambo haupo kwa mujibu wa sheria.

Aidha Magala amesema kushiriki mafunzo ya Mgambo si lazima bali ni hiari ya mtu mwenye kujitokeza na kujiandikisha ili kuwa mkakamavu na kupata walinzi wazuri wa amani katika jamii.

Ndugu Magala amewataka wana mafunzo ya mgambo kuwa mstari wa mbele na kuwa mfano katika kutekeleza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za nchi kwa kuwa na nidhamu kama wanajeshi wengine mara watakapomaliza mafunzo hayo.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia faida watakazopata mara baada ya kumaliza mafunzo ya mgambo ni pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi kupitia mpango wa ulinzi shilikishi/Polisi jamii katika maeneo mbalimbali mjini na vijijini, kupewa kipaumbele pale ajira za wanajeshi zinapotolewa na kupata ajira katika makapuni ya ulinzi:

Baada ya kufungua mafunzo ya mgambo Mkuu wa Wilaya ya Newala ametembelea shule ya Sekondari ya Mnyambe na kuikagua na kujionea maendeleao ya shule hiyo ya mnyambe.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
VIONGOZI
Viongzoi wa kata za mayanga na naumbu wametakiwa kuhakikisha kuwa wnakuwa mstari wa mbele katika kuboresha kiparto kwa wananchi wao
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndugu Wilmani Kapenjama Ndile alipokuwa anazungumza na viongozi hao mapema leo
Ndugu Ndile amesema kuwa viongozi wanapaswa kuhakikisha wanaboresha hali ya uchumi kwa wananchi wao kwa kuhakikisha kuwa wanawatautia soko la mazao yaom wanayoyazalisha
Amesema kuwa kwa muda mrefu wananchi wa mtwara wamekuwa wanategemea zaidi zao la korosho kuwakomboa kimaisha na hivyo ameshauri kulimwa zao mbadala ambalio linasoko la uhakika ili kuondoa umaskini na utegemezi wa zao moja kwa wakulima hao
Mkuu huyo wa wilaya yupo katika ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na kuona maeneo ya kufanyia kazi tangu alipoteuliwa na Rais Kikwete kuwa mkuu wa wilaya ya mtwara.

No comments: