Monday, July 16, 2012

DLAMINI-ZUMA.... ASHINDA UCHAGUZI TUME YA MUUNGANO WA AFRIKA


Nkosazana Dlamini-Zuma, kutoka Afrika Kusini, ameshinda uchaguzi mkali kuwa kiongozi mpya wa Tume ya Muungano wa Afrika.
Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, alimshinda kiongozi wa Tume hiyo anayeondoka Jean Ping wa Gabon, katika uchaguzi mkali uliopigwa mara kadhaa.
"hivi sasa tunaye kiongozi wa Tume ya Muungano wa Afrika Madam Zuma, ambaye sasa ataongoza siku za usoni za taasisi hii," ndivyo alivyosema Rais wa Benin Thomas Boni Yayi ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU.
Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 63, ni balozi mwenye ujuzi na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru nchini Afrika Kusini wakati wa Ubaguzi wa rangi.
Yeye ni daktari wa mwanadamu na amewahi kuhudumu kama Waziri wa Afya, Maswala ya Nchini na waziri wa Mashauri ya nchi za Kigeni nchini Afrika Kusini. BBC
Alikuwa mke wa zamani  wa Rais wa sasa wa Afrika Kusini

No comments: