Tuesday, June 19, 2012

NJEMBA YASHIRIKIANA NA NDUGU ZAKE KUMBAKA MKEWE

Mkazi wa Kijiji cha Mbugani mkoani Mara, Cliford Mgeta anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kushirikiana na ndugu zake, kumbaka mkewe hadi kumpotezea fahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Absalom Mwakyoma alisema Mgeta na ndugu zake wawili; Teka na Kenyakoro ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Mgeta Mgeta, walishirikiana kufanya kitendo hicho Juni 2 saa 1.30 usiku.

“Baada ya watuhumiwa hawa kutenda kosa hilo, mwanamke huyo alipoteza fahamu na alikimbizwa katika hospitali ya mkoa ambako alipata matibabu na kuruhusiwa lakini watuhumiwa wote watatu tumewakamata kwa mahojiano zaidi,” alisema Kamanda Mwakyoma.

Kamanda alisema siku hiyo Mbugani, ndugu hao watatu walishirikiana kwa awamu kumbaka mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32 (jina limehifadhiwa).

Kamanda Mwakyoma alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia leo kujibu mashitaka yanayowakabili.

Kutokana na tukio hilo, Mwakyoma aliomba wananchi wa mkoa huo hasa wanaume kuacha vitendo vya kudhalilisha wake zao kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Source: http://www.wavuti.

No comments: