Sunday, June 24, 2012

MSOMI WA MAWASILIANO YA UMMA... LEONARD MAPULI AJIULIZA SABABU YA TANZANIA KUTUMIA NOTI MBILI

Mwaka jana mwezi wa kwanza,BOT iliidhinisha matumizi ya noti mpya badala ya zile zilizokuwepo.
Noti hizo ziliingizwa kwenye mzunguko wa pesa,kwa kudhamiria kuondoa zilizokuwepo kabisa,na kufanya mpya zichukue nafasi yake,lakini cha kushangaza,mpaka sasa,Tanzania bado inatumia noti hizo kwa pamoja na katika mzunguko mmoja.

Nchini Uganda,mwezi wa tano mwaka 2010,BOU iliidhinisha matumizi ya noti mpya,na iliichukuwa Benki hiyo mwezi mmoja tu baadae kondoa kabisa noti zote za zamani na kubakiza mpya pekee.

Sasa BOT imeshindwa nini kuziondoa noti hizi za zamani na kuruhusu mpya kuchukua nafasi?Wachumi mpo wengi nchi hii,lakini mmekaa kimya tu bila kuueleza madhara ya jambo hilo katika muhimili mzima wa uchumi nchini...

Serikali ina waziri wa fedha sasa sijui kama kazi yake ni kuandaa bajeti tu,au vipi, basi aitwe waziri wa bajeti tu na si wa fedha....Gavana wa Benki kuu yupo tu,na cha ajabu kuna mtu kaajiliwa BOT kwa kazi ya kuchoma pesa ambazo hazifai,je anafanya kazi gani sasa?

Haya,cha ajabu kingine ni kwamba,zile noti mpya za 500,1000,2000,5000,na 10000 ndio za ajabu na zimeshachakaa sasa utadhani ndio za zamani,hii ndo Tanzania,Jamhuri pekee ya Muungano duniani,lakini pia nchi pekee yenye pesa aina mbili katika money circulation moja duniani...


KWA HERUFI KUBWA,NALAZIMIKA KUSEMA KUWA,MFUMO MBOVU WA SERIKALI,INAYOONGOZWA NA RAIS KIKWETE,NDIO CHANZO CHA YOTE HAYA MADUDU,NA KUWA WAMESHAONA WATANZANIA HATUJUI KITU,NA HATUNA TABIA YA KUHOJI MAMBO YA MSINGI,KWANI WENGI WETU NI WAOGA.

Leonard Mapuli,SAUT,MWANZA.

No comments: