Wednesday, June 20, 2012

BREAKING NEWSSSS...... DROGBA AHAMIA CHINA KLABU YA SHANGHAI SHENHUA


Mwamba huyo ametia kandarasi ya miaka miwili-na-nusu na timu hiyo ya China.
Kujiunga na klabu hicho , kimemfanya awe timu moja na mchezaji mwengine wa Chelsea Nicolas Anelka.
Drogba mwenye umri wa miaka 34 amesema kabla ya kuamua kuhamia China alifikiria kwa makin sanai.
"Nilitilia maanani mialiko chungu nzima niliopata katika kipindi cha wiki chache zilizopita , lakini nafikiri kwa wakati huu kuhamia timu ya Shanghai Shenhua ulikuwa uamuzi mzuri"
Mwamba huyo wa Ivory Coast atakumbukwa kwa bao alilofungia Chalsea walipocheza na Bayern Munich ya Ujerumani.Bao hilo liliifanya Chalsea ijiandikie historia ya kushinda kombe la Klabu bingwa bara Ulaya.
Drogba alijiunga na Chalsea mwaka wa 2004 kutoka Olympic Marseille ya Ufaransa kwa pauni million 24. Alikuwa baadhi ya wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Meneja Jose Mourinho alipojiunga na Chalsea.
Akiwa Chalsea kwa kipindi cha miaka minane, Drgoba aliisaidia klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Uingereza mara tatu na kombe la FA mara nne.
Mwamba huyo wa Ivory Coast anaondoka Chalsea akiwa ameandikisha historia ya kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 157 hivyo kuwa mchezaji nambari nne katika kwa ufungaji wa magoli katika historia ya Chalsea.
Katika kujiunga kwake na timu hiyo ya Shanghai Shenhua , Drogba anasema jukumu lake la kwanza ni kufanya soka ya China itambulike duniani.
Chanzo BBC...
KWENYE PAGE YAKE YA FACEBOOK"Today I can inform you that I have signed with Chinese club Shanghai Shenhua FC for a two and a half year deal" - Read more: http://bit.ly/MszXt1
872 ·  · 

No comments: